My Blog List

Friday, September 3, 2010

KIKAO CHA KAZI KATI YA VIONGOZI KUTOKA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NA WATENDAJI KATIKA HALMASHAURI ZOTE ZA WILAYA MKOANI MTWARA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bw.Anatoli Tarimo akifungua rasmi kikao cha kazi kati ya viongozi wa mfuko wa taifa wa bima ya afya na watendaji katika halmashauri zote za Mkoa wa Mtwara, mambo haya yalifanyika katika ukumbi wa Veta.

WATENDAJI WA MIFUKO YA JAMII WANOLEWA


Na.Godwin Msalichuma,

Mtwara.

WATENDAJI wa mifuko ya afya ya jamii katika halmashauri zote sita za Wilaya katika Mkoa wa Mtwara wamehimizwa kuwa chachu ya mabadiliko ili jamii iweze kuchangamkia fursa inayotolewa na mifuko hiyo katika maeneo yao waweze kudumisha afya bora ili kujiletea maendeleo .

Rai hiyo ilitolewa katika ufunguzi wa kikao cha pamoja cha kazi kilichokaa hivi karibuni katika ukumbi wa Veta mjini hapa kati ya viongozi wa mifuko hiyo kitaifa na watendaji wote na wakuu wa Wilaya kutoka katika halmashauri za Mkoa wa Mtwara mwenyekiti wao akiwa mkuu wa Mkoa Bw.Anatoli Tarimo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi Bw.Tarimo alisema kuwa suala la afya ni la muhimu sana katika jamii yoyote katika kuleta maendeleo yake na hii ilikuwa ni kuonyesha kwa watendaji hao kuwa jinsi jamii inavyotakiwa kuelimishwa na kuongozwa katika masuala hayo .

“Watendaji wenzangu tuanze kwa kuionyesha jamii kuwa masuala ya afya ni muhimu zaidi kuliko kitu kingine, kwani bila afya iliyo bora hakuna maendeleo…tuwahimize basi waitumie hiyo mifuko ya afya ya jamii kuboresha jamii zao ili tuendeleze kilimo kwanza kama vile Serikali inavyosema” alisema Bw.Tarimo.

Alisema kuwa kuugua kwa mkuu wa kaya mke au mume kunavuruga mpango mzima wa shughuli za familia za kila siku na hali inakuwa mbaya zaidi pale familia inapokuwa haina fedha za kugharimia matibabu, ndipo Serikali ilipoamua kuanzisha mifuko hiyo ili kupunguza kero kwa wananchi.

Mwanzoni katika hutoba ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa taifa wa bima ya afya Bw.Emmanuel Humba alisema kuwa ujio wao ni kuhakikisha watendaji na viongozi katika halmashauri za Wilaya wanaweka njia bora ya kuimarisha mifuko ya afya ya jamii na kuongeza kuwa.

Lengo lao linguine ni kuona kuwa kunakuwa na namna ya kuboresha huduma ya mifuko hiyo katika halmashauri zote hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo tutajenga afya bora katika jamii zetu na kuleta maendeleo kwa ujumla.








Baadhi ya washiriki wa kikao hicho katika ukumbi wa Veta Mtwara

No comments:

Post a Comment

Any