TUKIO KUBWA LA MICHEZO LA KIHISTORIA KUSINI
Na Godwin Msalichuma,
Mtwara,
MOJAWAPO ya matukio ya kimichezo ambayo huwa yanadhaniwa na Kampuni ya bia Tanzania TBL la mpira wa miguu KILI TAIFA CUP limeacha historia kubwa katika Mikoa yetu ya kusini mwa Tanzania.
Tukio hili limeifanya timu ya Mkoa wa Lindi kufika fainali za kinyang’iro hicho ambacho kilizishirikisha timunne katika kituo cha Mtwara ambazo ni Ruvuma, Mtwara, Lindi na Ilala ambao walikuwa mabingwa watetezi wa kombe hilo.
Hapa nitawaonyesha katika picha matukio ya kukabidhiana vifaa vya michezo siku moja kabla ya kuanza mashindano hayo ambayo yalitimua vumbi katika kituo cha Mtwara kuanzia Mei 07, mwaka huu.
Mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, Mkoa wa Mtwara na Lindi Bw.Mohamed Mbiku aliyeketi katikati, wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo na wawakilishi wa timu zinazocheza Kili Taifa Cup itakayoanza kesho katika uwanja wa umoja kituo cha Mtwara, pembeni kulia kwake ni Bi.Tamika Chikawe kutoka kampuni ya Executive Solution na kushoto kwake ni mwakilishi wa Chama cha Mpira wa miguu kutoka Mtwara Bw.Vicent Majiri.(Picha na Godwin Msalichuma)
Mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ta Bia ya Tanzania TBL, Mkoa wa Mtwara na Lindi Bw.Mohamed Mbiku akitoa maelezo kwa Waandishi wa habari (hawako kwenye picha) jinsi ya mashindano ya Kili Taifa cup yatakavyoendeshwa. Picha na Godwin Msalichuma.
Mwakilishi wa kikosi cha Ilala Bw.Mbuguni Andrew kushoto akipokea jezi kutoka kwa mwakilishi wa mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL Bw.Mohamed Mbiku. Picha na http://msalichuma.blospot.com
Kocha wa kikosi cha Mtwara Bw.Said Mnunduma kushoto akipokea jezi kutoka kwa afisa wa TBL.
Mwakilishi wa kikosi cha Ruvuma Bw.Hassanali Mohamed kushoto akipokea jezi kotoka kwa afisa wa TBL.
Meneja wa kikosi cha Lindi Bw.Seif Sinani kushoto akipokea jezi kutoka kwa afisa wa TBL.Picha na Godwin Msalichuma
No comments:
Post a Comment
Any