TAMASHA LA NNE LA MAKUYA KUFANYIKA MTWARA
Na Godwin Msalichuma,
Mtwara,
KWA MUJIBU wa Maelezo ya Mkurugenzi mwenza wa
Shirika la (ADEA) Kituo cha Maendeleo Kupitia Uchumi na Sanaa cha mjini Mtwara
watafanya tamasha la nne kuanzia Novemba 17 na 18, mwaka huu katika uwanja wa
kumbukumbu ya Nangwanda Sijaona mjini hapo.
Bw. Philipo Lulale alibainisha kuwa Shirika lake
linajitahidi kuboresha maisha ya wasanii wakiwemo Wachoraji, Wasusi, Mafundi
chuma na Wachoraji katika eneo la Kusini mwa Tanzania kupitia mafunzo
mbalimbali wanayoyatoa kituoni hapo.
ADEA inajitahidi kufanya yote hayo wakiangalia sera
ya utamaduni inasema nini juu ya tasnia
ya sanaa, ukiipitia inabainisha kuwa ukiangalia katika zama hizi za Teknolojia
katika utamaduni jamii inaweza kufanya ubunifu wa vifaa au zana, stadi mbinu na
taratibu za kufikiri na kutenda ili kudumisha uhai na kuboresha hali ya maisha
ya binadamu na mazingira yake.
Shirika lake tokea kuanzishwa kwake mwaka 2004
limeweza kuwakusanya makabila matatu makubwa katika Mkoa wa Mtwara ambayo ni
Wamakonde, Wamakuwa na Wayao ambapo wameunda neno moja linalojulika kama
(MAKUYA) na kufanya kujulika kama tamasha la MAKUYA.
Aidha ukizingatia sera ya utamaduni inasema kuwa
Tanzania hivi sasa inatumia Teknolojia za aina mbili ya jadi na ya kisasa
ambapo zote zinatumika sambamba na zinaingiliana na ingefaa zote ziendelezwe na
hapo ndipo ADEA wanapoingia kuwatoa mashaka wale wanaosema tamasha la utmaduni
lina maana gani na umuhimu gani katika jamii ya sasa.
Hata hivyo Shirika hilo linaamini kuwa utamaduni ni
elimu kwa mujibu wa sera yake hiyo ambapo jamii inapata ujuzi na uzoefu kupitia
huo na kuurithisha kwa jamii na vizazi vijavyo kwa lengo la kukidhi mahitaji ya
kundi hilo.
Awali ya yote kabla hajamaliza kutoa maelezo yake
alimkaribisha Bw. Dominic Chonde mratibu wa tamasha ambapo alibainisha kuwa
tamasha hilo limegawanyika katika makundi ambapo wapo wacheza ngoma za asili,
maonyesho ya wazi ya mafundi wa jadi, banda kwa ajili ya vifaa vya jadi na
michezo mbalimbali ya jadi.
Alifafanua kuwa kutakuwa na vikundi kumi na vitano
vya ngoma kutoka katika Wilaya za Mkoa wa Mtwara ambapo alitumia fursa hiyo
kwakaribisha wananchi wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani na nje ya
Mkoa huo kuja kutembelea tamasha hilo kwani halina kiingilio na ni mchango wa
jamii katika utamaduni wa nchi yetu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
Any