WAMACHINGA ARUSHA WACHAKURA WAVAMIA KIWANJA NA KUJIPIMIA MAENEO YA KUFANYIA BIASHARA
Wafanyabiashara
ndogo ndogo maarafu kama machinga jijini Arusha 27 septemba wamevamia
eneo la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la kilombero baada
ya kubomoa uzio wa eneo hilo na kisha kuanza kugawana maeno ya
kufanyiabiashara kwa kujipimia
Wamachinga wamama wakiwa wanajipimia maeneo ya kufanyia bishara kama inavyo onekana katika picha
Hali hiyo
ilisababisha Vurugu jana katika jiji la Arusha wakati ugeni wa watu
mbalimbali kutoka nchi za Afrika wakiwa hapa kwaajili ya mkutano mkubwa
wa mapinduzi ya kijani
Hatahivyo,katika
vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha wananchi(Cuf),Bw.Athuman
Abrahaman alishambuliwa kwa mawe na kisha kujeruhiwa eneo la usoni na
watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema huku gari la matangazo la
Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa mawe na spika zake kuharibika
vibaya.
Askari wa jiji la
Arusha walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita na gari lao katika
maeneo mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia wamachinga wote
kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara zao.
Askari
hao walikuwa wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo
ambayo hayajatengwa kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo
wakikahidi watachukua bidhaa zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za
kisheria.
Hatahivyo,baada ya
muda mfupi ndipo askari hao walianza kutekeleza majukumu yao ya kusomba
bidhaa hizo na kisha kuzipakia ndani ya gari lao huku wakivipeleka
katika ofisi za manispaa ya Arusha.
Hatua
hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya kwa pamoja na kisha
kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa mabati
uliokuwepo na kisha kuanza kujigawia maeneo kwa kuyapima kwa kamba.
Baadhi ya wamachinga
walisema kuwa eneo walilohamishiwa awali eneo la NMC haliwafai kwa
shughuli zao kwakuwa miundombinu hakuna katika eneo hilo sambamba na
kutokuwepo usalama wa mali zao wakiwa katika biasharta zao
“Hatuondoki hapa
mpaka kieleweke,,tumehoka kunyanyaswa bila kupewa haki zetu,,,hapa
tulipo tunafamilia zinatutegemea sana”sauti zilisikika
Hata hivyo wamachinga
hao walienda mbali kwa kudai kuwa eneo walilopelekwa haliwatoshi
kwakuwa hata walipopelekwa eneo hilo kuna baadhi ya wamachinga walikosa
eneo la kufanyia biashara
Wamachinga hao zaidi
ya 200 walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo kupora mali
mbalimbali zilizopo ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na saruji
zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo
Katika heka heka za
kugawana viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao walikata miti
iliyokuwemo ndani na kisha kuanza kuichoma kwa moto hali ambayo
ilisababisha wingu zito la moshi kutanda hewani.
Hatahivyo,wakati
tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa wamesheheni kwenye magari yao
walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo hilo lakini hawakuonekana
wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia wamachinga hao.
Kitendo cha askari wa
jeshi la polisi mkoni hapa kushindwa kuwadhibiti wamachinga hao
kimetajwa kimetokana na uhaba wa askari kutokana na ugeni wa mkutano wa
AGRA pamoja na kuhofia hali ya amani kuharibika jijini Arusha.
Mkuu wa wilaya ya
Arusha,John Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba wamachinga hao
wamevamia eneo hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku akikitupia lawama
chama kimoja cha siasa hapa nchini kwamba kimehusika katika kuhamasisha
vurugu hizo.
Alisema kwamba kwa
sasa watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa kuwa wana ugeni
mkubwa lakini alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kupiga mawe
gari la Cuf na mfuasi wake si cha kiungwana.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole
alisema kwamba kitendo cha wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja
sheria na wataondolewa hapo hivi karibuni.
Mkombole,mbali na
kulaani tukio hilo alisema kwamba uongozi wa jiji umepanga maeneo
mbalimbali ya kufanyia biashara na eneo hilo ni mali ya mtu binafsi
ambapo alikuwa ameanza jitihada za kuliendeleza
|
STORI NA PICHA ZOTE KWA MSAADA WA JAMII BLOG |
No comments:
Post a Comment
Any