Mwenyekiti CCM Mtwara: Sitagombea
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Alhaji Dadi Mbulu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo (Agosti, 27,2012) ofisini kwake Mbulu alisema hana mpango wa kutetea kiti chake kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili.
Mbulu ambaye alisema katika kipindi cha uongozi wake hatasahau alivyosakamwa na baadhi ya wanachama wake kwa kutoa ‘kifungoni’ mbunge wa Mtwara Mjini Hasnain Murji baada ya kufungiwa na viongozi waliopita wa chama hicho alisema.
“Nimechuja …Nimepata maamuzi kutoendelea kutetea kiti changu…kubwa zaidi afya yangu, pia kama kiongozi lazima niwe na moyo wa kuridhika, nimekuwa mwenyekiti wa halmashauri na meya kwa miaka 11 na mwenyekiti wa CCM kwa miaka Mitano, sasa inatosha”
Aliongezakuwa “Hakuna shinikizo kutoka kwa mtu yeyote…katika kipindi
Alishauri kuwa ni vema kwa wagombea kujiepusha na kampeni za kuchafuana kwani zinaweza kusababisha mgawanyiko wa chama hata baada ya uchaguzi.
“Kuna dalili za kuchafuana….huko kufilisika kisiasa, wasitumie nafasi hiyo kuchafua majina ya wengine…jieleze utakifanyia nini chama na si kushambulia wagombea wenzako” alisema Mbulu
Habari kwaniaba ya Kusini blog
No comments:
Post a Comment
Any