‘Housegirl’ auawa kinyama Dar
JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam linamshikilia kijana Yuda Paul
(30), mkazi wa Kisiwani Kigamboni, kwa tuhuma za mauaji ya mfanyakazi
wa ndani, Flora Tadei, ambaye alimzika katika uwanja wa tajiri yao.
Akizungumza na NIPASHE jana jijini Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23 mwaka jana akiwa nyumbani kwa tajiri yake huko Kigamboni.
Kamanda alisema Flora alikuwa ni mfanyakazi wa ndani katika eneo hilo na pia ni mkazi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara na mtuhumiwa huyo alikuwa ni mfanyakazi bustani katika nyumba hiyo.
Alisema wakiwa wanafanya kazi kwa pamoja, siku ya tukio mtuhumiwa na marehemu waliachwa nyumbani na bosi wao aliyekuwa ameenda kazini ambapo Paul alimuua marehemu huyo na kumzika kwenye uwanja wa tajiri yao.
Hata hivyo, Kamanda alisema baada ya tukio hilo mtuhumiwa alijenga mazingira ya kuonyesha kuwa marehemu alimuibia tajiri huyo na kutoroka kwani alichukua baadhi ya vitu ndani ya nyumba na kwenda kuvitupa porini.
Akiendelea kusimulia tukio hilo, alisema mke wa bosi wao aliporejea kutoka kazini aliamini kuwa ni kweli marehemu huyo amemuibia na kuamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kigamboni.
Alisema toka kipindi hicho mpaka sasa wameamini kuwa marehemu amewaibia na anatafutwa na polisi huku ndugu wa marehemu wakijua kuwa ndugu yao ni mzima na anafanya kazi Kigamboni.
Kamanda Misime alisema polisi inaendelea na uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kuufufua mwili wa marehemu huyo ambao umekutwa umeshaoza na kubakia mifupa.
Alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwa ajili ya kusubiriwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi.
Kamanda alisema ndugu wa marehemu huyo bado hawajapatiwa taarifa juu ya kifo hicho kwani wanajua ndugu yao anaendelea na kazi.
Alisema uchunguzi dhidi ya tukio hilo bado unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.