My Blog List

Tuesday, February 8, 2011

SHEREHE YA KUMKARIBISHA TAG SHANGANI BW. NA BI. LUCAS MALUHA SHEREHE YENYEWE ILIFANYIKIA KOROGWE TANGA

 Bwana harusi na bibi harusi Lucas na Rabecca wakitoka katika kanisa la TAG miracle center baada ya kukalibishwa kwa nderemo na vifijo wakitokea Korogwe Tanga walikofanyia harusi yao.
 Wakishuhudia muandalizi wa keki yao akiwaandalia ili wajikumbushe tena kiapo chao mbele ya washirika wa Shangani TAG miracle center.
 Wakiwa na tabasamu la uhakika bw. na bibi Lucas ambaye ni mtumishi katika Banki ya NMB Mtwara na jiko lake likiwa pale MTUWASA nadhani pia wanatafakari maisha yao baada ya kutoka katika ukumbi huu.
 Wakiwa na furaha kubwa na kushindwa kuamini kinachotokea mbele yao, bwana na bibi Lucas wakisubiri kukaribishwa viti ili tafrija ianze.
 Mchungaji George wa kanisa la TAG shangani pamoja na msaidizi wake wakishuhudia shamra shamra za kuwakaribisha maharusi hawa.
 La ajabu alilolifanya bw. Lucas ni kwamba Mungu hakumpa mke tu bali hata chombo cha usafiri, hapa washirika wakiliweka wakfu gari hilo.
Hili lilikuwa tukio jingine la mshirika wa shangani kujaliwa na Mungu kupata chombo cha usafiri, na hapa mchungaji George wa kanisa la TAG Shangani akiongoza washirika kuliweka wakfu gari hilo.

No comments:

Post a Comment

Any