My Blog List

Friday, September 3, 2010

TRA MKOANI HAPA WAZINDUA KLABU ZA KODI KATIKA SHULE ZA SEKONDARI KUMI HALMASHAURI YA MANISPAA YA MTWARA

Wanafunzi wa shule za Sekondari wakifuatilia matukio katika uzinduzi wa klabu za kodi katika shule zao Manispaa ya Mtwara Mikindani

Meza kuu katika ukumbi wa Veta siku ya uzinduzi wa klabu za kodi katika shule za Sekondari Manispaa ya Mtwara.
Wanafunzi katika uzinduzi wa klabu za kodi Veta Mtwara

Kikundi cha sanaa wakitoa burudani siku ya uzinduzi wa klabu za kodi shule za Sekondari katika ukumbi wa Veta Mtwara

TRA WAZINDUA KLABU ZA KODI MASHULENI


Na.Godwin Msalichuma,

MAMLAKA ya mapato Mkoani hapa kupita idara yake ya elimu kwa mlipa kodi imezindua klabu za kodi katika shule kumi za Sekondari zilizopo katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara ili kutoa elimu kwa walipa kodi wa sasa na baadae kwa lengo la kuinua uelewa wa masuala hayo katika jamii.

Hayo yamejitokeza hivi karibuni katika ukumbi wa Veta mjini hapa na kuhudhuriwa na baadhi ya wanafunzi na walimu walezi wa klabu hizo kutoka katika shule zote kumi, wakiongozwa na maafisa wa Mamlaka na Meneja msaidizi Bw.Rashid Herith kuwa mgeni rasmi.

Katika hotuba yake ya uzinduzi rasmi Bw.Herith alisema mamlaka ya mapato Tanzania inaamini kuwa wanafunzi ni kundi kubwa na muhimu katika jamii ambao wana kiu ya kufahamu mambo mbalimbali ya kodi na hamu hiyo inaongezeka siku hadi siku.

“Ndugu washiriki wa hafla hii tuliona kuwa kundi hili likifikiwa tutajenga wigo mpana wa uelewa wa masuala ya kodi katika jamii ,lakini pia wao wanaweza kuwa walimu wazuri katika jamii wanazotoka kwani wakielewa vizuri huwa hawasiti kuwaelimisha wenzao” alisema Bw.Herith.

Meneja huyo msaidizi alisema kuwa kutokana na ari kubwa ya kutaka kuelewa masuala ya kodi miongoni mwa wanafunzi, mamlaka ya mapato imelazimika kuchukua jukumu la kuanzisha vilabu hivyo vya kodi na kuongeza kuwa.

Sababu zingine zikiwa kuwaandaa walipaji wa baadaye wakiwemo watalaam wa kodi na kuwafanya wanachama wa vilabu hivyo waweze kutoa elimu kwa wenzao ndani na nje ya mazingira ya shule na pia kutoa hamasa kwa jamii juu ya umuhimu wa ulipaji.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Any