My Blog List

Monday, June 7, 2010

Habari kutoka Mtwara

ZAIN YASAIDIA SHULE ZA SEKONDARI MTWARA

Juni 05, 2010,

Na Godwin Msalichuma,

Mtwara.

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zain Tanzania Mkoani hapa imetoa vitabu kwa Sekondari nne za Mkoa wa Mtwara na Lindi vyenye thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 4, katika mpango wake wa BON (Build Our Nation) shule hizo ni Mtwara wasichana, sekondari ya kutwa Njengwa za Mtwara pamoja na shule ya Nakiu na Kineng’ene za Mkoa wa Lindi.

Akikabidhi vitabu hivyo katika shule ya sekondari wasichana, Afisa elimu wa Mkoa wa Mtwara Bw.Hipson Kipenya alisema kuwa lengo la Zain la kutoa vitabu kwa wanafunzi ni kusaidia jitihada za serikali katika kujikwamua kielimu na kuzidi kuiboresha zaidi ili kufikia maendeleo ya melania.

Aifafanua kuwa mradi huo wa Zain ni msaada mkubwa ambao unalenga kusaidia shule za sekondari ambazo zitaweza kuhudumia wanafunzi wake hali ambayo itaipunguzia mzigo serikali kwani wengi tunajua kuwa inamajukumu mengi ambayo inakabiliwa nayo.

“Pokeeni vitabu hivi kwani ni hazina kubwa katika kutafuta elimu….nadhani vitawaongezea juhudi katika masomo yenu……nategemea mtavitunza na kuvitumia vizuri ili wengine nao watakao kuja wavikute baada ya nyinyi kumaliza masomo hapa shuleni….ila naomba sana mvisome hivyo vitabu kwani wengi wenu mmetoka mbali kuja kusoma hapa Mtwara kwahiyo vitabu ndiyo hivyo sasa kazi kwenu kuvisoma na kuvitunza”alisema Bw.Kipenya.

Akipokea msaada huo wa vitabu kwa niaba ya shule zote nne Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bi.Mary Kaguo aliishukuru Kampuni hiyo kwa kusaidia shule hapa Tanzania na kuwataka wanafunzi kutumia vema vitabu hivyo.

Rose Makinda ambaye ni Dada Mkuu wa shule ya wasichana ya Mtwara alishukuru kwa niaba ya wenzake na aliahidi kuvitumia vema vitabu hivyo walivyopatiwa ili lengo lililokusudiwa liweze kutimia na kuiomba shule kuwasimamia ili viweze kudumu kwa muda mrefu zaidi na kufanya wengine watakaokuja wanufaike na msaada huo.

“Wengi mnajua shida ya uhaba wa vitabu ilivyokuwa inatusumbua hapa shuleni……sasa Zain wametukomboa kwahiyo tuna matumaini ya kufanya vizuri katika mitihani yetu ya kumaliza masomo yetu kwa wale wa Kidato cha nne na sisi wa Kidato cha sita….ila jukumu letu kubwa kuvitumia vizuri ili wadogo zetu nao waweze kuvitumia pale watakapopata nafasi ya kuja kusoma hapa Mtwara” alisema Makinda.

Mwisho.

Afisa elimu wa Mkoa wa Mtwara Bw.Hipson Kipenya akikabidhi vitabu kutoka Kampuni ya Zain Tanzania kwa Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mtwara Bi.Mary Kaguo, Makabidhiano hayo yalifanyika shuleni hapo. (Picha na Godwin Msalichuma).

Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana ya Mtwara Bi.Mary Kaguo akikabidhi vitabu kutoka Kampuni ya Zain Tanzania kwa Dada mkuu wa shule Rose Makinda kwa niaba ya wanafunzi wote. (Picha na Godwin Msalichuma).

Afisa elimu wa Mkoa wa Mtwara Bw.Hipson Kipenya aliyeketi katikati, katika hafla ya makabidhiano ya vitabu kutoka Kampuni ya Zain Tanzania, Kushoto ni Meneja wa Kampuni hiyo Bw.Bartholomeo Masatu na kulia ni Mkuu wa shule ya sekondari ya wasichana Bi.Mary Kaguo. (Picha na Godwin Msalichuma).

Wengi wanaweza kusema ni kanisa au banda la kufugia mifugo!la hasha hii ni mashine ya kusaga nafaka kwa ajili ya chakula cha binadamu,ipo katika mtaa wa sabasaba Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani.(picha na Godwin Msalichuma)

WIZARA KUTOA MILIONI 214 MSANGAMKUU

Na Godwin Msalichuma,

Mtwara.

WIZARA ya maendeleo ya mifugo na uvuvi imetenga kiasi cha shilingi milioni 214 kwa ajili ya wakazi wa Msangamkuu kijiji kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, ili ziweze kutumika katika miradi ya Macemp katika kulinda hifadhi ya bahari na maliasili zilizoko katika Bahari ya Hindi imefahamika.

Hayo yalisemwa hivi karibuni katika ziara aliyoifanya Waziri wa Wizara hiyo Bw.John Magufuli alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhala kijijini hapo, baada ya wanakijiji kumwuliza hatima yao baada ya kusalimisha nyavu zao ambazo zilikatazwa na serikali kwani si nzuri katika uvuvi endelevu.

“Wananchi wenzangu wa Msangamkuu serikali imeliona hilo ndiyo maana Wizara yangu imeshatoa kiasi hicho cha fedha ili muache uvuvi usioendelevu……jmani yetu kuwa fedha hizo siyo ndogo na kama kuna kikundi hakijapata naomba mnipe taarifa mapema ili tumwulize mratibu wa miradi hiyo ya Macemp ndiyo maana nimekuja naye leo hapa” alisema Magufuli.

Ziara hiyo aliongozana pia na Waziri wa nchi menejementi ya utumishi wa umma Bi.Hawa Ghasia katika salamu zake kwa wananchi hao kwanza aliwapa pole kwa ajali iliyotokea katika kivuko cha kuelekea kijijini hapo ambapo watu wawili walipoteza maisha yao na wengine saba kunusulika.

Aliongeza na kusema hayuko mbali nao kwani serikali imeshatenga fedha kwa ajili ya vivuko viwili ambavyo kimoja kwa Msangamkuu na kingine katika kijiji cha Kilambo katika kuvuka mto Ruvuma.

“Ninacho wahakikishia ni kwamba serikali imeshaweka bajeti kwa ajili ya vivuko hivyo viwili ambavyo mapema vitapatikana baada ya kupatikana kwa mzabuni wa kuendesha hiyo biashara ya kuvuka…..kwahiyo ondoeni shaka hizo ajali zitakuwa historia kwenu, lakini nawaomba wale wote wanaofanya biashara ya vivuko kwa sasa waangalie usalama wa wavukaji kwa kutumia vyombo vyenye injini na vilivyosajiliwa kisheria ili kupunguza hatari wakati wa kuvuka”alisema Bi.Ghasia.

Alifafanua kuwa anaongea kwa uhakika kwa kuwa hata Bw. Magufuli aliyeongozana naye katika ziara hiyo alishawahi kuiongoza Wizara ya miundombinu na hata baadhi ya watendaji katika Wizara hiyo aliwapendekeza yeye mwenyewe kwa mkono wake.

“Jamani wananchi wenzangu Bw. Magufuli ni huyu hapa kama naongea uongo aseme…..nadhani naye atalisimamia na kuona mnapata vivuko hivyo ili kuweza kujikwamua kimaendeleo”aliongeza Waziri huyo.

Mwisho.

,Ni jengo la ofisi za hifadhi ya bahari na maliasili zinazotokana na bahari ya Hindi (Marine Parks) lililojengwa katika kijiji cha Msimbati Mkoani Mtwara ambalo Waziri John Magufuli alilifungua rasmi hivi karibuni. (picha na Godwin Msalichuma)

1 comment:

Any