Dkt. Mponda kulia akiwa na Bw. John Julius wa asasi isiyokuwa ya kisrikali ROSDO Masasi-waikiwa katika ukumbi wa mikutano Naliendele siku ya mkutano wa wadau wa Karanga |
Kazi na dawa, wakati wa kupasha matumbo siku ya mkutano wa wadau wa karanga hivi karibuni katika kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo na mifugo Naliendele Mtwara |
Mkuu wa kituo cha utafiti Naliendele Dkt.Elly Kafiriti akifuatilia mkutano wa wadau wa karanga
Hapa akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari hawapo pichani
Stori yenyewe:
WASHAURIWA KUTUMIA KANUNI BORA ZA KILIMO
Na Godwin Msalichuma,
Mtwara,
WADAU wa kilimo cha karanga Mkoani hapa wameshauriwa
kutumia kanuni bora za kilimo na uvunaji wake ili kupunguza athari za
maambukizi na kuenea kwa sumu kuvu (aflatoxin) ili kuongeza mauzo katika soko
la ndani na nje ya nchi.
Ushauri huo ulitolewa na mtafiti wa mbegu za mafuta
Dkt. Shomari Mponda wa kituo cha Utafiti wa mbegu za kilimo na mifugo cha
Naliendele Mkoani Mtwara katika kikao cha wadau wa zao la karanga
kilichofanyika hivi karibuni kituoni hapo.
Alisema tatizo la sumu kuvu lipo katika mazao
mbalimbali ya nafaka kama mahindi, muhogo, karanga na mtama, lakini katika
karanga hukumbwa zaidi kwasababu uzalishwaji wake huanzia katika udongo pale
mkulima atakapofanya uzembe kipindi cha kukalibia mavuno na kama kuna dalili za
ukame tatizo huwa kubwa.
Hata hivyo aliwashauri kuwa kama kutakuwa na dalili
za ukame wakulima wanapaswa kunyanyulia udongo katika mashina ya mikaranga ili
kutunza unyevu kuzuia zisiweze kupasuka zikiwa ardhini kwani huko ndiko kuna
vimelea vya sumu hiyo ambavyo husababishwa na aina fulani za uyoga.
Alishauri njia zingine za kukabiliana na sumu hiyo
ni kukausha vizuri karanga baada ya kuvunwa ili kupunguza unyevu ambao mara
nyingi husababisha ueneaji wa athari hizo, vilevile kuzitunza katika majunia
yanayopitisha hewa vizuri.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt. Elly
Kafiriti alisema kuwa ni muhimu wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo na
uvunaji wa karanga kwani wasipofanya hivyo maambukiza ya sumu kuvu ni hatari
kwa afya za watumiaji wake kwani kwa watoto wadogo huathiri ukuaji wao, huleta
utindio wa ubongo na jinsi unavyokua kuanzia miaka 35 na kuendelea huleta
saratani ya ini na kuongeza kuwa:
Inaathiri soko letu la nje kwa kuzirudisha karanga
zetu au kutoa fedha kidogo ambazo huwa ni hasara kubwa kwa wakulima na nchi kwa
ujumla, hivyo amewaomba wakulima na wadau wa zao la karanga kuwa makini katika
kuvuna na kuziandaa kwa ajili ya matumizi na biashara ya zao hilo ndani na nje
ya nchi.
No comments:
Post a Comment
Any