SEKTA YA ELIMU MTWARA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO
Godwin Msalichuma,
Mtwara,
SEKTA ya elimu Mkoani Mtwara inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo za mimba,utoro ,mahudhurio hafifu hususani katika shule za sekondari sambamba na upungufu wa walimu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake hivi karibuni afisa elimu Mkoa wa Mtwara Bw.Hipson Kipenya alisema kuwa jumla ya kesi 40 za mimba zilizowasilishwa katika kipindi cha miezi 5(Januari hadi Mei 15) mwaka huu kwa shule za sekondari, ambapo hata hivyo tatizo hilo limeoneka kupungua katika kila mwaka.
Bw.Kipenya alisema kuwa kupungua kwa tatizo hilo la mimba linatokana na jitihada zilizofanywa na serikali kwa kushirikiana na jamii husika katika kuhakikisha tatizo linakwisha na kwamba mwaka 2009 mimba 53 zilizowasilishwa kwa shule za sekondari, na kwa shule za msingi ziliripotiwa kesi 87 ambapo kwa 2010 shule za msingi hakukuwapo na kesi hata moja.
Aidha afisa elimu huyo alizungumzia suala la utoro ambapo alisema kuwa jumla ya wanafunzi 1107 wamekuwa hawahudhurii masomo ipasavyo ambapo kati ya hao wanafunzi yatima ni 601 na wanafunzi 506 wanaishi katika mazingira magumu.
“Sekta ya elimu imekuwa ikifanya kila jitihada za kuwafuatilia wazazi na walezi katika kuhakikisha watoto wao wanahudhuria masomo… na kila halmashauri tumeziagiza kuhakikisha zinatenga bajeti za kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu,”alisema Bw.Kipenya
Pia alisema kuwa halmashauri katika mkoa huo zimekuwa zikielemewa na ongezeko la watoto wanaoishi katika mazingira magumu na kuongeza kuwa jumla ya watoto 5765 wanaishi katika mazingira hayo na wamekuwa wakipatiwa misaada ya ada ya shule,chakula,malazi pamoja na sare za shule.
Alisema halmashauri za wilaya ya Mtwara Mikindani ina jumla ya watoto 1259, Newala watoto 3360,Masasi watoto 122,Tandahimba jumala ya watoto 250 Mtwara vijijini watoto 276 na Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu ina watoto 490.
Vile vile katika upungufu wa walimu, Bw.Kipenya alisema mkoa unakabiliwa na upungufu wa walimu wa shule za msingi mahitaji ni walimu 7336, waliopo 577 upungufu ni 2242 sawa na asilimia 30.6.
Katika shule za sekondari alisema mahitaji ni walimu 2528, waliopo 816 na upungufu ni walimu 1732 sawa na asilimia 68.53 na hatua mbalimbali zimekuwa zikichukuliwa ili kukabiliana na tatizo hilo la upungufu wa walimu.
Alisema upungufu huo unatokana na baadhi ya walimu kutowasili katika vituo vya kazi au wengine kuwasili vituoni na kisha kuondoka na hiyo ni kutokana na ukosefu wa huduma muhimi za kijamii ikiwemo Usafiri,maji,afya na ukosefu wa nyumba za walimu.
Mwisho
ZINGATIENI UBORA WA BIDHAA ZENU
Na Godwin Msalichuma, Mtwara
WAJASIRIAMALI wadogo wanaojihusisha na usindikaji wa vyakula na matunda mkoani Mtwara wametakiwa kuacha kutafuta mchawi wa biashara zao na badala yake wameshauriwa kuzingatia ubora ili kulinda soko la bidhaa wanazozalisha.
Ushauri huo umetolewa mwishoni mwa wiki na mbunge wa viti maalum mkoani Mtwara, Bi.Anasitazia Wambura alipokuwa akifunga mafunzo ya usindikaji wa mazao ya nafaka na matunda kwa kikundi cha Kunicha Self Help group yaliyotolewa na shirika la kuhudumia viwanda vidogo (Sido) Mkoani hapa
Alisema tatizo kubwa la ukosefu wa soko la uhakika la bidhaa za wajasiriamali wanaojihusisha na usindikaji wa vyakula na matunda ni kushuka kwa ubora wa bidhaa wanazozalisha hali inayowakimbiza walaji wa bidhaa hizo.
“Leo mmetengeneza mvinyo mzuri
Alisema kwa kuzingatia ubora wa bidhaa wanazozalisha kutawawezesha kuwa kileleni kibiashara na kwamba tatizo la ukosefu wa wateja litakuwa historia kwao ambapo pia aliwashauri kuzitangaza bidhaa hizo ili zifahamike na watu wengi kwa lengo la kukuza soko.
Awali akisoma taarifa katibu wa Kunicha, Bi.Aziza Myao alisema kikundi hicho chenye wanachama 22 wengi wao wanawake wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa masoko ya bidhaa wanazozalisha, vitendea kazi na mitaji hali inayodhorotesha shughuli za kikundi.
“Mhe. Mgeni rasmi, kikundi chetu tulikianzisha Mei, 5, 2010….hadi sasa tuna wanachama 22 na akiba ya sh. 440,000 zilizotokana na michango ya wanachama na tayari taratibu zote za usajili zimekamilika” alisema Bi.Myao
Meneja wa sido Mkoa wa Mtwara Bw.Norvatus Lihepanyama alisema mbali na mafunzo ya usindikaji wa vyakula na matunda pia wanakikundi hao wamepatiwa elimu ya ujasiriamali itayowawezesha kuendesha biashara zao kwa faida.
“Mgeni rasmi, changamoto ya sido Mkoani hapa ni ufinyu wa bajeti yetu, hali hii inatusababisha tushindwe kuwafikia watu wengi wanaoishi vijijini…tumekuwa tukitoa mafunzo kwa wajasiriamali wa mjini kwa kiasi kikubwa” alisema Bw.Lihepanyama.
Mwisho
No comments:
Post a Comment
Any