My Blog List

Saturday, May 14, 2016

Msalichuma Mtwara news: Changamkieni fursa katika Visiwa vya ‘marashi’,

Msalichuma Mtwara news: Changamkieni fursa katika Visiwa vya ‘marashi’,

Picasa pictures

Changamkieni fursa katika Visiwa vya ‘marashi’,

Na Godwin Msalichuma, Mtwara,

WAFANYABIASHARA katika Mkoa wa Mtwara wametakiwa
kuchangamkia fursa za biashara zinapopatikana katika nchi ya Comoro ili
kudumisha ujirani mwema baina ya nchi mbili hizo.

Hayo yamesemwa na balozi wa nchi hiyo hapa Tanzania,
Dr.Ahamada El Badaoui Mohamed, alipokuwa akiwasilisha mada ya fursa
zinazopatikana nchini kwake katika mkutano mkuu wa 27 wa mwaka wa chama cha
wenye viwanda, biashara na kilimo Tanzania, (TCCIA), Mkoani Mtwara katika
ukumbi wa Hotel ya Tiffany Dimond.

Alisema ziko fursa nyingi nchini kwake katika sekta
za kilimo, uvuvi na utalii ambapo zinahitaji wawekezaji kutoka Comoro na nje ya
nchi hiyo kwani anaamini kuwa bila kuruhusu uwekezaji kutoka nje wanaweza
wasipige hatua wanayotaka kuifikia kimaendeleo.

“Tunafurahishwa na kauli mbiu ya mheshiwa, John
Magufuli ya kusema hapa kazi tuu na kweli sasa tunataka Comoro na Mtwara iwe
hapa kazi tuu maneno tuyaweke pembeni ili tuweze kukuza uchumi wa nchi zetu kwa
kuruhusu uwekezaji kutoka nje na hapa tuanze na nyinyi majirani zetu” alisema
Mohamed.

Alisema katika kilimo wanahitaji mazao kama ya
Mpunga, Karafuu na Vinnila, lakini pia aliongeza kuwa katika Mifugo wanahitaji
tani 3,000 kwa mwaka kama kuna inayeweza kuchangamkia hiyo fursa, hata hivyo
alisema maziwa, mayai na Karanga zinahitaji kwa wingi, mfano mwaka 2013
tuliagiza tani 52 kwa mwaka.

Aliongelea pia kuhusu sheria, taratibu na kanuni za
uwekezaji katika nchi yake zimelegezwa sana kiasi kwamba kwa muda wa siku moja
unaweza kupata usajili wa biashara yako na biashara ikaendelea bila shida
kabisa.

Kwa upande wake, Ally Mgangawe, mfanyabiashara wa
Mtwara na ni mwanachama wa TCCIA, ambaye tayari ameshajitosa kufanya biashara
na nchi hiyo, alisema kuwa ameshafanikiwa kwenda kupeleka mboga mboga za aina
mbalimbali na kupata soko zuri na la uhakika kabisa na mpaka sasa anapokea
maulizo ya bidhaa hizo kwa simu.

“Mimi namshukuru Mungu nimeshafanya safari nne
kwenda Comoro na hupeleka mboga mboga kweli soko lipo na ni zuri lakini kuna
changamoto ya usafiri kwa sisi wafanyabiashara wadogo lakini niliweza kwenda na
Jahazi la takribani tani 10 na kufanikiwa kufanya biashara nzuri” alisema
Mgangawe.

Alisema kuwa serikali inajitahidi kuweka mazingira
mazuri kwa wafanya biashara nchini lakini shida inakuja kwa baadhi ya watendaji
wa serikali wasio waaminifi haswa kwa upande wa ulinzi na usalama ambapo
huingilia mambo wasiyoyajua na kuyatolea maamuzi ambayo mara huwa siyo ya
busara.

Hata hivyo, Chilangala Abdalah, mfanyabiashara wa
Mtwara na mwanachama wa TCCIA katika Mkoa huo, alisema TCCIA wanajitahidi
kuweka mazingira mazuri ya fursa za kibiashara zinazotokea katika Mkoa huo
hivyo kuweka usawa kwa wanachama wao na hata wasio wanachama.

“Napenda kuwashukuru TCCIA, maana wemeweka mazingira
mazuri katika kugawa fursa za kibiashara zinapotokea maana huwa wanazitangaza
kwa wanachama wote hivyo basi mwenye uwezo wa kuchangamkia anafanya hivyo na
mara nyingine hata wasio wanachama hupata fursa mbalimbali kutoka kwa taasisi
hii ya kibiashara” alisema Chilangala.



Awali akifungua Mkutano huo, katibu tawala wa Mkoa
wa Mtwara, Alfred Luanda, aliwasisitiza wafanyabiashara wa Mkoa huo kutumia
tekinolojia ya habari na mawasilia na bila kusahau mitandao ya kijamii katika
kuvumisha biashara zao ili kuweza kupata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi.

Thursday, June 19, 2014

TAG SHANGANI MIRACLE WAADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 75 YA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD TANZANIA

Shughuli mbalimbali zilizofanyika kuanzia tarehe 14/06 mpaka 15,06 katika maadhimisho ya jubilee ya miaka 75 ya kanisa la TAG Tanzania, katika kanisa hili la TAG Shangani Miracle tample Mtwara mjini.

PSI MTWARA YAKUTANA NA WASAMBAZAJI WA BIDHAA ZAKE

Picasa pictures
Picasa pictures
afya ya mama na mtoto visiwani victoria mashakani

Afya ya mama na mtoto ziwa Victoria shakani

Afya ya mama na mtoto mashakati ziwa victoria

Tanzania creative industries network (TACIN) kufanya tamasha Mtwara 16-17, Agost 2014

Mwenyekiti mtendaji Anic Kashasha, akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa safari lounge Mtwara, juu ya jinsi tamasha la Mtwara fesival likavyofanyika hapo mwezi wa nane mwaka huu.

Tuesday, January 14, 2014

Picasa pictures
Mambo ya ziwa Tanganyika upande wa nchi ya Burundi