My Blog List

Sunday, September 2, 2012

HABARI ZA KUSIKITISHA KUTOKA MKOA WA IRINGA, MAUAJI HAYA YATAENDELEA MPAKA LINI?

Mwenzetu Daud Mwangosi Hatunaye Tena


 Habari kwa msaada wa Mjengwa blog:
Ndugu zangu,

Jioni ya leo nikiwa katikati ya kufundisha soka ya vijana hapa Iringa nilipigiwa simu na ndugu yangu Allen,  Katibu Wa CHADEMA , Iringa,  akinitaarifu tukio la vurugu zilizotokea Nyololo, Mufindi na hata kifo cha Mwanahabari mwenzetu, mpiganaji  Daud Mwangosi ambaye pia  ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari hapa Iringa. Kuondoka kwake kutaacha pengo kubwa. Inasikitisha sana.  Ni juzi tu nilikutana na kusalimiana nae nje ya ofisi zake kwenye jengo la Mwamoto.

Pole zangu binafsi kwa familia yake ya karibu na mbali.  Tuko nao katika wakati huu mgumu kwao.
Chini hapa ni baadhi ya picha nilizopata kumpiga Daud Mwangosi katika uhai wake.
Maggid Mjengwa,
Iringa
0788 111 765

Gazeti La Nyakati Kumbe Laweza Kujirekebisha!



Nimeandika mara kadhaa na hapa narejea tena hadi nikiona kuwa  wahusikawanaanza kuelewa.wiki hii gazeti la nyakati kidogo limeacha kuhubiri ushetani wa freemason na japo bado hawajaacha kabisa lakini walau hawana habari kubwa mbele wiki hii ikitukuza Abrakadabra.Na kama vile mapunguwani gazeti jingine tena nalo likijiita la kikristo la msema kweli linaanza upuuzi uleule.Jamani tusiwaunge mkono wakomunisti waliposema dini ni bangi.
Ludovick

Taswira Za Vurugu Zilizotokea Leo Nyololo, Mufindi

Picha : Francis Godwin

MWANDISHI DAUD MWANGOSI AUAWA JIONI HII


 ( Pichani Daud Mwangosi akiwa kazini muda mfupi kabla kufikwa na mauti yake.)

Hii hapa ni taarifa kutoka kwa Francis Godwin,
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa

Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote . Chanzo:Francis Godwin na Mjengwa blog Iringa

No comments:

Post a Comment

Any